Kuhusu katalogi

Watumiaji wa programu ya WhatsApp Business wanaweza kushiriki bidhaa na huduma zao na wateja kwa kuunda katalogi, ambayo huonyeshwa kwenye jalada la biashara zao.
Kila bidhaa au huduma kwenye katalogi ina jina la kipekee pamoja na sehemu za hiari kujaza:
  • Bei
  • Maelezo
  • Kiungo cha tovuti
  • Msimbo wa bidhaa
Maelezo haya huwasaidia wateja kutambua bidhaa kwenye katalogi. Katalogi inaweza kuwa na bidhaa hadi 500.
Katalogi iliyosasishwa huwawezesha wateja kutafuta bidhaa au huduma za biashara na kuwasiliana na biashara. Wateja wanaweza kushiriki bidhaa za katalogi na marafiki zao au kutuma ujumbe kwa biashara ili kuuliza maswali.
Kidokezo cha Biashara: Kusasisha katalogi yako ya bidhaa na huduma mara kwa mara kunaweza kufanya biashara yako iendelee kuvutia na kuwezesha mteja kusalia.
Kushiriki katalogi huruhusu biashara ndogo kusambaza katalogi zao na kufikia wateja watarajiwa. Watumiaji wa WhatsApp Business wanaweza kutuma katalogi kamili kwa wateja ambao tayari wanaowasiliana nao. Wanaweza pia kushiriki kiungo chao cha katalogi mahali popote, kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mengine, hivyo kuwezesha wateja wengi watarajiwa kugundua biashara zao na kutuma ujumbe kwao moja kwa moja kuhusu bidhaa na huduma zao.
Kumbuka: Kuweka bei kwenye katalogi kunapatikana katika baadhi ya nchi pekee.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La