Jinsi ya kufanya ununuzi unapopiga soga na biashara

Baadhi ya biashara hushiriki orodha ya hadi bidhaa 30 zilizo kwenye katalogi zao ili kuendana na maombi wanapopiga soga na wateja. Kufanya hivi kunaweza kurahisisha kupata bidhaa unayotaka.
Kufanya ununuzi unapopiga soga na biashara
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Nenda kwenye kichupo cha Soga > gusa soga kati yako na biashara.
 3. Unaweza kugusa aikoni ya kitufe cha ununuzi (
  au
  ) karibu na jina la biashara ili kufikia katalogi yote ya biashara hiyo au kutuma ujumbe ili kufanya biashara ijue ni bidhaa gani unatafuta.
  1. Weka ujumbe wako kwenye soga. Gusa TUMA
   .
  2. Ikiwa biashara inatumia orodha, inaweza kushiriki orodha ya zinazowezekana. Gusa orodha hiyo.
 4. Kutoka kwenye katalogi au orodha, gusa
  karibu na bidhaa ili uongeze bidhaa hiyo kwenye kikapu chako. Unaweza pia kugusa bidhaa ili ufungue ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo. Kisha, gusa WEKA KWENYE KIKAPU.
  • Gusa
   au
   ili kuongeza au kupunguza idadi ya bidhaa hiyo kwenye kikapu chako.
 5. Gusa ANGALIA KIKAPU au aikoni ya Kikapu (
  au
  ).
 6. Gusa Weka ujumbe ikiwa unataka kutuma ujumbe mfupi pamoja na kikapu chako. Kisha, gusa TUMA KWA BIASHARA
  .
Baada ya biashara kupokea oda yako, mtajadili namna ya malipo.
Rasilimali zinazohusiana
Kuhusu kununua kwenye WhatsApp
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La