Tunasasisha Sera yetu ya Faragha kwa watu walio katika Eneo la Ulaya

Tunasasisha Sera yetu ya Faragha kwa watumiaji wetu, jinsi tulivyoagizwa na mdhibiti wetu mkuu wa ulinzi wa data katika eneo la Ulaya. Mdhibiti huyo ni Tume ya Ulinzi wa Data Ayalandi.
Kama kawaida, hatuwezi kusoma au kusikiliza mawasiliano yako ya binafsi, kwa sababu yanafumbwa mwisho hadi mwisho. Hili halitabadilika kamwe.

Tunajua kuwa faragha ni jambo kuu sana kwa watumiaji wetu, kwa hivyo tunataka kueleweka vizuri zaidi: sasisho hili halibadilishi jinsi tunavyoendesha huduma zetu, ikiwa ni pamoja jinsi tunavyochakata, kutumia au kushiriki data yako na kampuni nyingine, ikiwemo kampuni yetu kuu ambayo ni Meta.
Badala yake, tumepanga vizuri Sera yetu ya Faragha na kuisasisha kwa kuongeza maelezo ya ziada, ikiwemo:
  • Jinsi tunavyotumia data: Tumeongeza maelezo zaidi kuhusu data tunayokusanya na kutumia, kwa nini tunaihifadhi na lini tunafuta data yako, pamoja na maelezo kuhusu huduma ambazo wahusika wengine hutupatia.
  • Utendaji wetu kimataifa: Tumeongeza maelezo zaidi kuhusu ni kwa nini tunashiriki data nje ya mipaka ili kutoa huduma zetu kimataifa, na jinsi tunavyolinda data hiyo.
  • Misingi tuliyo nayo kisheria kuchakata data: Tumeongeza maelezo zaidi kuhusu misingi ya kisheria tunayotegemea ili kuchakata data yako.
Tunataraji utaendelea kufurahia kutumia WhatsApp.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La