Jinsi ya kuhakiki ujumbe wa sauti

Kwa kuhakiki rasimu ya sauti uliyorekodi kabla ya kuituma, unaweza kutuma ujumbe wako ukiwa na ujasiri.
Kuhakiki ujumbe wa sauti
Unaweza kusikiliza ujumbe wako wa sauti kabla ya kuutuma.
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Bofya maikrofoni
  halafu uanze kuzungumza.
 3. Mara umalizapo, bofya acha
  .
 4. Bofya cheza
  ili usikilize ulichorekodi. Unaweza pia kubofya sehemu yoyote ya sauti uliyorekodi ili uicheze kutoka hapo.
 5. Bofya debe la taka
  ili kufuta ujumbe huo wa sauti, bofya ENDELEA ili uendelee kurekodi, au bofya tuma
  ili kuutuma.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La