Kuhusu viungo vinavyotiliwa shaka

Android
iPhone
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Mac
Kwa baadhi ya viungo unavyopokea kwenye soga, unaweza kuona kiashirio cha kiungo kinachotiliwa shaka.
Kiashirio hiki kinaweza kuonekana wakati kiungo kina mchanganyiko wa herufi ambazo huchukuliwa kuwa si za kawaida. Watumaji wa ujumbe taka hutumia michanganyiko ya herufi ili kukuhadaa uguse viungo. Viungo hivi vinaweza kuonekana kuwa vinaelekeza kwenye tovuti halali, lakini kwa hakika vinakuelekeza kwenye tovuti hasidi.
Huu hapa mfano wa kiungo cha kutiliwa shaka:
https://ẉhatsapp.com/free-tickets
Kumbuka: Herufi ya kwanza inaonekana kuwa herufi "w" lakini ni herufi "ẉ." Hii ina maana kuwa mtumaji wa ujumbe taka anaweza kuwa amekuhadaa utembelee tovuti ambayo haihusiani na WhatsApp.
Unapopokea viungo, kagua kwa makini maudhui ya ujumbe huo. Ikiwa kiungo kimewekwa alama ya kutiliwa shaka, unaweza kugusa kiungo kisha ujumbe ibukizi utaonekana. Ujumbe utaangazia herufi zozote zisizo za kawaida kwenye kiungo. Kisha unaweza kuchagua kufungua kiungo hicho au kurudi kwenye soga.
WhatsApp hufanya ukaguzi wa kiotomatiki ili kubaini ikiwa kiungo ni cha kutiliwa shaka. Ili kulinda faragha yako, ukaguzi huu hufanyika kikamilifu kwenye kifaa chako. Kumbuka, kwa sababu ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, WhatsApp haiwezi kuona maudhui ya ujumbe wako.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwa salama kwenye WhatsApp, soma makala haya.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La