Majibu ya maswali yako kuhusu sasisho la Sera ya Faragha ya WhatsApp la Januari 2021

Mnamo Januari 2021 tulianza kutoa sasisho la Sera ya Faragha na tumepokea maswali mengi yenye umakini. Kwa sababu ya uvumi unaosambazwa, tungependa kujibu baadhi ya maswali yanayoulizwa sana ambayo tumeyapokea. Huwa tunajitahidi sana kubuni WhatsApp kwa namna inayowasaidia watu kuwasiliana kwa faragha.
Tunapenda kubainisha waziwazi kwamba sasisho hili la sera haliathiri faragha ya ujumbe mnaotumiana na ndugu na marafiki kwa namna yoyote ile. Mabadiliko haya yanahusu vipengele vya hiari vya biashara kwenye WhatsApp na yanatoa ufafanuzi zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya na kutumia data. Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele vipya vya biashara na sasisho la Sera ya Faragha ya WhatsApp hapa.
Faragha na usalama wa ujumbe wako wa binafsi
Hatuwezi kuona ujumbe wa binafsi au kusikiliza simu zako, Meta pia haiwezi: WhatsApp wala Meta haziwezi kusoma ujumbe au kusikiliza simu kati yako na marafiki, familia na wafanyakazi wenza kwenye WhatsApp. Chochote mnachoshiriki, hubakia kati yenu. Hii ni kwa sababu ujumbe wako wa binafsi hulindwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho. Hatutawahi kamwe kudhoofisha ulinzi huu na huwa tunabainisha kwenye kila soga ili ufahamu kujitolea kwetu. Pata maelezo zaidi kuhusu usalama wa WhatsApp hapa.
Hatuhifadhi kumbukumbu za kila mtu anayetumiwa ujumbe au kupigiwa simu: Ingawa kwa kawaida watoa huduma na waendeshaji huhifadhi taarifa hizi, tunaamini kwamba kuhifadhi rekodi hizi kwa watumiaji bilioni mbili kunaweza kuwa hatari kwa faragha na usalama na hatufanyi hivyo.
Hatuwezi kuona mahali unapopashiriki, Meta pia haiwezi: Unaposhiriki mahali ulipo na mtu kwenye WhatsApp, taarifa zako za mahali hulindwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, kumaanisha kwamba hakuna mtu mwingine anaweza kuona mahali ulipopashiriki isipokuwa watu ulioshiriki nao.
Hatushiriki anwani zako na Meta: Ukituruhusu, tunaweza tu kufikia namba za simu kutoka kwenye kitabu cha anwani cha simu yako ili kufanya mawasiliano yawe ya haraka na ya uhakika na hatushiriki orodha yako ya anwani na programu nyingine zinazotolewa na Meta.
Vikundi vitasalia kuwa vya faragha: Tunatumia ushiriki kwenye vikundi kuwasilisha ujumbe na kulinda huduma yetu dhidi ya taka na matumizi mabaya. Hatushiriki taarifa hizi na Meta kwa madhumuni ya matangazo. Isitoshe, soga hizi za binafsi zimefumbwa mwisho hadi mwisho kwa hivyo hatuwezi kuziona.
Unaweza kufanya ujumbe utoweke: Kwa faragha ya ziada, unaweza kuchagua kufanya ujumbe wako utoweke kwenye soga baada ya kuutuma. Pata maelezo zaidi kuhusu hili kwenye makala haya ya Kituo cha Msaada.
Unaweza kupakua data yako: Unaweza kupakua na kuona taarifa tulizo nazo kwenye akaunti yako moja kwa moja kutoka kwenye programu. Pata maelezo zaidi kwenye makala haya ya Kituo cha Msaada.
Utumaji ujumbe wa kibiashara na jinsi tunavyofanya kazi na Meta
Kila siku, mamilioni ya watu kote duniani huwasiliana na biashara za ukubwa mbalimbali kwa njia salama kwenye WhatsApp. Tunataka kuboresha na kurahisisha mawasiliano haya ukichagua kuwasiliana na biashara. Tutakuwa tukibainisha kwenye WhatsApp kila wakati unapowasiliana na biashara yoyote inayotumia vipengele hivi.
API ya Wingu inayopangishwa na Meta: Mawasiliano kati yako na biashara huwa tofauti na unapowasiliana na marafiki au familia. Baadhi ya biashara kubwa huhitaji huduma za kupangisha ili kudhibiti mawasiliano yao. Ndiyo maana tunazipa biashara chaguo la kutumia huduma salama za upangishaji zinazotolewa na Meta ili ziweze kudhibiti soga za WhatsApp na wateja wao, kujibu maswali, na kutuma taarifa muhimu kama vile stakabadhi za ununuzi. Lakini ikiwa unawasiliana na biashara kwa simu, barua pepe au WhatsApp, inaweza kuona unachosema na inaweza kutumia taarifa hizo kwa madhumuni yake ya mauzo, ambayo yanaweza kujumuisha utangazaji kwenye Meta. Ili kuhakikisha kwamba unafahamu, tunabainisha kwa uwazi ukiwa unafanya mazungumzo na biashara ambayo imechagua kutumia huduma za upangishaji zinazotolewa na Meta.
Kugundua biashara: Unaweza kuona tangazo kwenye Facebook likiwa na kitufe cha kutumia biashara ujumbe kupitia WhatsApp. Ikiwa una WhatsApp kwenye simu yako, utakuwa na chaguo la kuitumia biashara hiyo ujumbe. Facebook inaweza kutumia ufahamu wa unavyoingiliana na matangazo haya ili kubinafsisha matangazo unayoona kwenye Facebook.
Malipo kwenye WhatsApp: Katika nchi ambako huduma ya Malipo inapatikana, WhatsApp ina sera tofauti za faragha ya malipo, unazoweza kuzipata hapa. Sera hizo za faragha haziathiriwi na sasisho hili.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La