Jinsi ya kuangalia taarifa za kusomwa

Alama za tiki huonyeshwa karibu na kila ujumbe utakaotuma. Kila moja inaashiria yafuatayo:
 • Ujumbe umetumwa.
 • Ujumbe uliwasilishwa kwenye simu ya mpokeaji au vifaa vyake vinginevyo vilivyounganishwa.
 • Mpokeaji amesoma ujumbe.
Kumbuka:
 • Alama ya tiki ya pili itaonekana wakati ujumbe umewasilishwa kwenye kifaa chochote cha mpokeaji kilichounganishwa, hata kama simu yake imezimwa.
 • Katika soga ya kikundi, alama ya tiki ya pili itaonekana wakati washiriki wote katika kikundi wamepokea ujumbe wako. Alama za tiki mbili za bluu zitaonekana wakati washiriki wote katika kikundi wameusoma ujumbe wako.
Maelezo ya ujumbe
Kwa ujumbe wowote unaoutuma, utaweza kuona skrini ya maelezo ya ujumbe, inayoonyesha maelezo ya wakati ujumbe wako uliwasilishwa, kusomwa au kuchezwa na mpokeaji. Mshiriki anapoondoka kwenye kikundi, skrini ya maelezo ya ujumbe bado itaonyesha maelezo ya asili ikiwa na washiriki wote, pamoja na mshiriki ambaye ameondoka kwenye kikundi.
Kuona skrini ya maelezo ya ujumbe:
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Chagua soga ya binafsi au ya kikundi > FUNGUA.
 3. Chagua ujumbe > Chaguo > Maelezo ya ujumbe > SAWA.
Skrini ya Maelezo ya Ujumbe huonyesha:
Imetumwa:
 • Ujumbe wako ulitumwa kwenye simu ya mpokeaji.
Imewasilishwa:
 • Ujumbe wako umewasilishwa kwenye simu ya mpokeaji au vifaa vilivyounganishwa, lakini mpokeaji hajauona.
Imesomwa:
 • Mpokeaji amesoma ujumbe wako au kuona picha yako, faili la sauti au video.
Umechezwa:
 • Mpokeaji amecheza ujumbe wako wa sauti.
Kukosa taarifa za kusomwa
Ikiwa huoni alama mbili za tiki za bluu, kipaza sauti cha bluu au maandishi "Imefunguliwa" karibu na ujumbe wako uliotumwa au ujumbe wa sauti:
 • Inawezekana kuwa wewe au mpokeaji wako mmezima taarifa za kusomwa kwenye mipangilio ya faragha.
 • Inawezekana mpokeaji amekuzuia.
 • Inawezekana simu ya mpokeaji imezimwa.
 • Inawezekana mpokeaji hajafungua mazungumzo yenu.
 • Inawezekana wewe au mpokeaji mna matatizo ya muunganisho.
Kuzima taarifa za kusomwa
Unaweza kuzima taarifa za kusomwa kwa soga za binafsi. Hatua hii haiwezi kuzima taarifa za kusomwa za soga za kikundi au taarifa za kusomwa kwa ujumbe wa sauti. Hakuna njia ya kuzima mipangilio hiyo.
 1. Fungua WhatsApp > bonyeza Chaguo.
 2. Chagua > Mipangilio > bonyeza SAWA.
 3. Chagua Akaunti > Faragha.
 4. Bonyeza Fungua.
 5. Chagua Taarifa za kusomwa.
 6. Bonyeza ZIMA.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La