Jinsi ya kuacha kuhifadhi media ya WhatsApp kwenye matunzio ya simu yako

Unapopakua faili ya media, itahifadhiwa kiotomatiki kwenye matunzio ya simu yako. Hiari ya Uonekanaji wa media imezimwa kwa kawaida. Kipengele hiki kinaathiri media mpya iliyopakuliwa mara kipengele kimewashwa au kuzimwa na haihusu media ya zamani.
Kuachisha media kuhifadhiwa kutoka kwa soga zako za kibinafsi na vikundi
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Nenda Hiari zaidi
  > Mipangilio > Soga
  .
 3. Zima Uonekanaji wa media.
Kuachisha media kuhifadhiwa kutoka kwa soga ya kibinafsi au kikundi
 1. Fungua soga ya kibinafsi au kikundi.
 2. Gusa Hiari zaidi
  > Tazama mwasiliani au Maelezo ya kikundi.
  • Mbadala, gusa jina la mwasiliani au mada ya kikundi.
 3. Gusa Uonekanaji wa media > Hapana > Sawa.
Kuunda faili ya .nomedia
Mbadala, unaweza kuunda faili ya .nomedia kwenye folda ya picha za WhatsApp. Tafadhali zingatia kwamba hii itaficha picha za WhatsApp kutoka kwa matunzio ya simu yako.
 1. Pakua uchunguzi wa faili kutoka kwa Duka la Google Play.
 2. Kwenye uchunguzi wa faili, nenda Images/WhatsApp Images/.
 3. Unda faili inayoitwa .nomedia, pamoja na nukta.
Ukitaka kutazama picha zako kwenye matunzio ya simu yako baadaye, futa tu faili ya .nomedia.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La