Imeshindwa kuhifadhi majibu ya haraka

Ikiwa huwezi kuhifadhi majibu yako ya haraka, angalia uhakikishe kuwa jibu hilo limefuata masharti yafuatayo ya umbo.
  • Idadi ya juu inayokubalika ya kuhifadhi majibu ya haraka ni 50.
  • Urefu wa juu wa njia mkato ya jibu la haraka ni herufi 25.
  • Njia mkato haziwezi kuwa na nafasi.
  • Njia zote mkato lazima zianze kwa mkwaju wa mbele /.
  • Idadi ya juu ya maneno msingi yanayoruhusiwa kwa kila jibu la haraka ni tatu.
  • Maneno ya msingi hayawezi kuwa na nafasi au herufi yoyote isiyo ya alfabeti au isiyo ya nambari.
  • Urefu wa juu wa neno moja la msingi ni herufi 15.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kutumia majibu ya haraka: Android | iPhone
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La