Kuhusu Vipengele vya Biashara

Tunapenda kubainisha waziwazi kwamba masasisho ya Januari 2021 ya masharti na sera ya faragha hayaathiri ujumbe wa binafsi. Mabadiliko haya yanahusiana na vipengele vya hiari vya biashara kwenye WhatsApp na yanatoa ufafanuzi zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya na kutumia data.

Ni kipi hakibadiliki?
Faragha na usalama wa ujumbe wako na simu zako za binafsi haubadiliki. Zimelindwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho na WhatsApp wala Meta haziwezi kusoma au kuzisikiliza. Kamwe hatutadhoofisha usalama huu na tunabainisha kila soga ili ufahamu kujitolea kwetu.
Vipengele vya Hiari vya Biashara
Tunajitahidi ili kuwahudumia ipasavyo zaidi ya watu milioni 175 ambao huwasiliana na akaunti za biashara kila siku. Masasisho haya yanayohusu vipengele vya hiari vya biashara ni sehemu ya juhudi zetu pana za kufanya mawasiliano na biashara yawe salama, bora na rahisi kwa kila mtu. Juhudi hizi ni pamoja na:
  • Kuwezesha huduma kwa wateja: Watu huona ni muhimu kupiga soga na biashara ili kuuliza maswali, kununua, au kupata taarifa muhimu kama vile stakabadhi za ununuzi. Sasa tunarahisisha mchakato wa kupiga soga na biashara ambazo zinaweza kutumia huduma za biashara za Meta. Ili kuwajibu wateja, baadhi ya biashara zinahitaji huduma salama za upangishaji ambazo Meta ina mpango wa kutoa. Biashara inapotumia huduma hii, tutabainisha kwa uwazi soga hiyo ili uamue kama utatuma ujumbe au la.
  • Kugundua biashara: Tayari watu wanaweza kugundua biashara kwenye Facebook au Instagram kutoka kwenye matangazo ambayo huonyesha kitufe unachoweza kubofya ili kutumia biashara ujumbe kupitia WhatsApp. Sawa na ilivyo katika matangazo mengine kwenye Facebook, ukichagua kubofya matangazo haya, yanaweza kutumiwa kubinafsisha matangazo unayoyaona kwenye Facebook. Usisahau, WhatsApp na Meta haziwezi kuona chochote kilichomo kwenye ujumbe uliofumbwa mwisho hadi mwisho.
  • Huduma za ununuzi: Watu wengi wananunua mtandaoni, hili linaongezeka hasa kwa vile tuko mbalimbali. Ambapo inapatikana, baadhi ya biashara zilizo na Duka kwenye Facebook au Instagram pia zinaweza kuwa na Maduka kwenye jalada la biashara la WhatsApp. Hili hukuruhusu kuona bidhaa za biashara zilizo kwenye Facebook na Instagram na kununua moja kwa moja kwenye WhatsApp. Ukiamua kuwasiliana na Maduka, tutakufahamisha kwenye WhatsApp jinsi data yako inavyoshirikiwa na Meta.
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu vipengele hivi vya hiari na jinsi tunavyofanya kazi na Meta hapa.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La