Jinsi ya kutuma GIF

Jinsi ya kutuma GIF
Unaweza kutuma GIF kwenye soga za binafsi au za kikundi kwenye WhatsApp.
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 3. Gusa Vibandiko
  > GIF.
 4. Kisha, unaweza kugusa:
  • Tafuta
   kutafuta GIF mahususi.
  • Hivi karibuni
   kuona GIF zako ulizotumia hivi karibuni.
  • Vipendwa
   kuona GIF zako unazozipenda.
 5. Chagua na gusa GIF unayotaka kutuma.
 6. Gusa Tuma
  .
Kuongeza GIF kwenye Vipendwa
Unaweza kuongeza GIF kwenye Vipendwa ili uweze kuzipata haraka baadaye.
 • Kuweka GIF katika vipendwa kutoka kwenye soga, gusa na ushikilie GIF iliyo katika soga ya binafsi au ya kikundi > gusa Nyota
  .
 • Kuweka GIF katika vipendwa kutoka kwenye menyu ya GIF, gusa na ushikilie GIF > gusa Ongeza kwenye Vipendwa.
Kuondoa GIF kwenye Vipendwa
 • Gusa Vipendwa
  > gusa na ushikilie GIF > gusa Ondoa kwenye Vipendwa.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La