Kuona "Inasubiri ujumbe huu. Hili linaweza kuchukua muda."
Wakati mwingine, unaweza kuona ujumbe ulio hapo juu badala ya uliotumiwa na unayewasiliana naye. Kutokana na ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, huenda ukahitaji kusubiri ujumbe wa mhusika ufike kwa sababu simu yake inahitajika kuwa mtandaoni. Hali hii inaweza kutokea ikiwa wewe au mtu unayepiga soga naye alisakinisha WhatsApp upya hivi karibuni au anatumia toleo la zamani.
Ili kuharakisha mchakato huu:
- Mwombe mtu mnayewasiliana afungue WhatsApp kwenye simu yake.
- Hakikisha kuwa nyote wawili mnatumia toleo la hivi karibuni la WhatsApp.
Kwa maelezo zaidi kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, tafadhali somawaraka wetu rasmi na makala haya.