Jinsi ya kutuma miitikio ya ujumbe

Unaweza kuitikia ujumbe katika soga zako binafsi na za kikundi ukitumia emoji. Unaweza kuona miitikio yote ya ujumbe kwa kugusa emoji ya miitikio chini ya ujumbe husika.
Kumbuka:
 • Unaweza kuweka mwitikio mmoja tu kwa kila ujumbe.
 • Miitikio kwenye ujumbe unaotoweka itatoweka wakati ujumbe husika unatoweka.
 • Haiwezekani kuficha miitikio au idadi ya miitikio.
 • Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla hujauondoa au kama uondoaji haujafanyika. Hutaarifiwa kama uondoaji haukufanyika.
Kuweka mwitikio kwenye ujumbe
Unapoweka mwitikio, ni mtumaji wa ujumbe unaoitikia pekee ndiye atapokea arifa.
 1. Bonyeza ujumbe kwa muda mrefu.
 2. Gusa ili uchague mojawapo ya emoji zinazoonyeshwa au gusa
  ili kuchagua emoji yoyote kutoka kwenye kibodi yako.
Kubadili mwitikio wako
Unaweza kubadilisha mwitikio wako kuwa mwingine.
 1. Bonyeza kwa muda mrefu ujumbe uliouitikia.
 2. Gusa emoji tofauti au gusa
  ili uchague emoji tofauti kutoka kwenye kibodi yako.
Kuondoa mwitiko
Unaweza kuondoa mwitiko wako kwenye ujumbe. Arifa haitatumwa kwa mtumaji wa ujumbe ikiwa utaondoa mwitikio.
 1. Bonyeza kwa muda mrefu ujumbe uliouitika au gusa mwitikio.
 2. Gusa emoji uliyoitika nayo ili uiondoe.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La