Kuhusu kuona nambari yako ya simu ikiwa tayari ipo kwenye WhatsApp

Akaunti zote za WhatsApp zinahusishwa na nambari ya simu ya mkononi. Kwa kuwa ni kawaida kwa nambari za simu kurejelezwa na watoa huduma za simu, inawezekana kuwa aliyekuwa mmiliki wa nambari yako ya simu ya sasa alikuwa akitumia WhatsApp.
Ikiwa mmiliki wa awali wa nambari yako ya simu hakufuta akaunti yake ya WhatsApp, wewe na unaowasiliana nao mnaweza kuona nambari yako ya simu kwenye WhatsApp kabla hujafungua akaunti mpya. Pia unaweza kuona picha ya jalada ya mtu mwingine na sehemu ya Kuhusu vikihusishwa na nambari yako ya simu.
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Hii inamaanisha tu kuwa akaunti ya awali haikufutwa, kwa hivyo taarifa za zamani bado ziko kwenye mfumo. Hii haimaanishi kuwa mmiliki wa awali wa nambari hiyo anaweza kufikia akaunti ya WhatsApp unayofungua kwa kutumia nambari yako mpya. Mazungumzo yako na data nyingine za WhatsApp ni salama.
Ili kusaidia kuondoa mkanganyiko unaotokana na nambari za simu zilizorejelewa, huwa tunafuatilia akaunti zisizotumiwa. Akaunti isipotumika kwa siku 45 na kisha ianze kutumika kwenye kifaa kingine cha mkononi, tunachukulia hili kuwa ishara kwamba nambari imerejelewa. Wakati huo, tutaondoa data ya akaunti ya zamani inayohusishwa na nambari hiyo ya simu - kama vile picha ya jalada na sehemu ya Kuhusu.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La