Jinsi ya kuagiza ukitumia kikapu

Unapotembelea katalogi ya biashara kwenye WhatsApp, tumia kitufe cha TUMIA BIASHARA UJUMBE ili kuanzisha mazungumzo au tumia kitufe cha ONGEZA KWENYE KIKAPU ili kuagiza bidhaa unayoangalia katika biashara husika.
Kuweka bidhaa kwenye kikapu
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Nenda kwenye soga yako au jalada la biashara ambako ungependa kuagiza bidhaa.
 3. Gusa Kitufe cha ununuzi
  karibu na jina la biashara ili ufikie katalogi ya biashara hiyo.
 4. Baada ya katalogi kufunguka, kagua bidhaa ambazo ungependa kuagiza.
 5. Gusa Ongeza bidhaa
  karibu na bidhaa ili uongeze bidhaa hiyo kwenye kikapu chako. Unaweza pia kugusa bidhaa ili ufungue ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo. Kisha, gusa WEKA KWENYE KIKAPU.
  • Gusa Ongeza bidhaa
   au Ondoa bidhaa
   ili kuongeza au kupunguza idadi ya bidhaa hiyo kwenye kikapu chako.
 6. Gusa WEKA KWENYE KIKAPU katika bidhaa ikiwa ungependa kuagiza.
Kumbuka: Unaweza pia kugusa TUMIA BIASHARA UJUMBE ili uulize kuhusu bidhaa. Ili kuuliza kuhusu bidhaa nyingi, ongeza zote kwenye kikapu kisha utume maswali yako katika ujumbe mmoja. Oda haijakamilika hadi lithibitishwe na muuzaji.
Kubadilisha bidhaa zilizo kwenye kikapu chako
 1. Gusa ANGALIA KIKAPU au
  ili uone bidhaa ulizoongeza kwenye kikapu chako.
 2. Gusa ONGEZA ZAIDI ili urudi kwenye katalogi kisha uongeze bidhaa zaidi.
 3. Gusa Ongeza bidhaa
  au Ondoa bidhaa
  ili kuongeza au kupunguza idadi ya bidhaa mahususi kwenye kikapu chako.
Kuagiza
 1. Baada ya kusasisha kikapu chako, gusa TUMA KWA BIASHARA.
 2. Baada ya kutuma, unaweza kuona maelezo ya oda yako kwa kugusa kitufe cha ANGALIA KIKAPU ULICHOTUMA katika dirisha la soga kati yako na muuzaji.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La