Â
Jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha
Kimsingi, WhatsApp huweka mipangilio yako ya faragha kurusuhu:
- Mtumiaji yeyote kuona picha ya jalada lako, maelezo kuhusu na taarifa za kusomwa
- Unaowasiliana nao kuona masasisho yako ya hali
- Mtumiaji yeyote kukuongeza kwenye vikundi
Kumbuka: Watumiaji uliowahifadhi kama anwani au ambao uliwatumia ujumbe hapo kabla wanaweza kuona mara yako ya mwisho kuona au kuwa mtandaoni.
Kubadilisha mipangilio ya faragha
- Kwenye:
- Android: Gusa Chaguo zaidi> Mipangilio > Faragha.
- iPhone: Gusa Mipangilio > Faragha.
- KaiOS: Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Akaunti > Faragha.
- Desktop: Bofya Menyu> Mipangilio > Faragha.
- Android: Gusa Chaguo zaidi
- Unaweza kubadilisha anayeweza:
- Kuona Mara yako ya Mwisho Kuonwa au Kuwa Mtandaoni
- Kuona Picha ya Jalada lako
- Kuona maelezo yako ya Kuhusu
- Kuona masasisho yako ya Hali
- Kuona Taarifa za kusomwa
- Kukuongeza kwenye Vikundi
Kumbuka:
- Usiposhiriki maelezo ya mara yako ya mwisho kuonwa au kuwa mtandaoni, hutaweza kuona maelezo ya mara ya mwisho watumiaji wengine walipoonwa au kuwa mtandaoni.
- Ukizima taarifa za kusomwa, hutaweza kuona taarifa za kusomwa kutoka kwa watumiaji wengine. Taarifa za kusomwa hutumwa kwa soga za vikundi kila mara.
- Ikiwa unayewasiliana naye amezima taarifa za kusomwa, hutaweza kuona ikiwa ameona sasisho lako la hali.
- Watu waliopo mtandaoni kwenye mazungumzo ya soga nawe wanaweza kuona unapoandika.