Â
Jinsi ya kuunda na kualika washiriki kwenye kikundi
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kuunda kikundi cha WhatsApp chenye hadi washiriki 1024.
Kuunda kikundi
- Nenda katika kichupo cha Soga kwenye WhatsApp.
- Gusa Soga Mpya> Kikundi Kipya.
- Ukiwa na soga iliyopo kwenye kichupo cha Soga, gusa Kikundi Kipya.
- Tafuta au uchague anwani ambazo ungependa kuongeza kwenye kikundi. Kisha, uguse Inayofuata.
- Weka jina la kikundi. Hili litakuwa jina la kikundi ambalo washiriki wote wataliona.
- Urefu wa jina usizidi herufi 100.
- Unaweza kuweka aikoni ya kikundi kwa kugusa aikoni ya Kamera. Unaweza chagua Kupiga Picha, Kuchagua Picha, Emoji na Vibandiko au Kutafuta kwenye Wavuti ili uweke picha. Baada ya kuweka, aikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye kichupo cha Soga.
- Gusa Unda unapomaliza.
Kualika kwenye vikundi kupitia viungo au msimbo wa QR
Ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi, unaweza kuwaalika watu wajiunge kwenye kikundi kwa kushiriki nao kiungo au msimbo wa QR. Msimamizi anaweza Kubadilisha kiungo ili kubatilisha kiungo cha mwaliko cha awali kisha aunde kiungo kipya.
- Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha uguse jina la kikundi.
- Au telezesha kushoto kwenye kikundi katika kichupo cha Soga. Kisha, uguse Zaidi > Maelezo ya kikundi.
- Gusa Alika kwenye Kikundi kupitia Kiungo.
- Chagua Tuma Kiungo Kupitia WhatsApp, Shiriki Kiungo, Nakili Kiungo au Msimbo wa QR.
- Ili kubadili kiungo, gusa Badili Kiungo > Badili Kiungo.
Kumbuka: Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unayeshiriki kiungo cha mwaliko naye anaweza kujiunga kwenye kikundi. Tumia kipengele hiki kwa watu unaowaamini pekee. Mtu yeyote ambaye amesambaziwa kiungo anaweza kujiunga kwenye kikundi bila idhini ya ziada kutoka kwa msimamizi wa kikundi.