Jinsi ya kuunda na kualika washiriki kwenye kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kuunda kikundi cha WhatsApp chenye hadi washiriki 256.
Kuunda kikundi
 1. Nenda kwenye kichupo cha Soga katika WhatsApp.
 2. Gusa Soga Mpya
  > Kikundi kipya.
  • Ikiwa una soga iliyopo kwenye kichupo cha Soga, gusa Kikundi Kipya.
 3. Tafuta au chagua watumiaji unaotaka kuwaweka kwenye kikundi. Kisha, gusa Inayofuata.
 4. Weka mada ya kikundi. Hili litakuwa jina la kikundi ambalo washiriki wote wataliona.
  • Ukomo wa mada ni herufi 25.
  • Unaweza kuweka aikoni ya kikundi kwa kugusa aikoni ya Kamera. Unaweza kuchagua Piga Picha, Chagua Picha au Tafuta Mtandaoni ili kuweka picha. Ukishaweka, aikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye kichupo cha Soga.
 5. Gusa Unda unapomaliza.
Kualika kwenye vikundi kupitia viungo
Ukiwa msimamizi wa kikundi, unaweza kuwaalika watu kujiunga na kikundi kwa kushiriki kiungo nao. Msimamizi anaweza Kubadilisha kiungo wakati wowote ili kubatilisha kiungo cha mwaliko wa awali na kuunda kiungo kipya.
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Vinginevyo, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha, gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
 2. Gusa Alika kwenye Kikundi kupitia Kiungo.
 3. Chagua Shiriki Kiungo, Nakili Kiungo au Msimbo wa QR.
  • Ili kuweka upya kiungo, gusa Weka upya Kiungo > Weka upya Kiungo.
Kumbuka:
 • Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unayemtumia kiungo cha mwaliko anaweza kujiunga na kikundi, kwa hivyo tumia kipengele hiki tu kwa watu unaowaamini. Inawezekana kwa mtu kusambaza kiungo kwa watu wengine, ambao wanaweza kujiunga na kikundi bila ruhusa ya ziada kutoka kwa msimamizi wa kikundi.
 • Tunaongeza ukubwa wa vikundi hatua kwa hatua katika miezi ijayo na huenda kukawa na kuchelewa kufikia kipengele hiki.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La