Imeshindwa kuunganisha kwenye WhatsApp

Ikiwa huwezi kutuma au kupokea ujumbe kwenye WhatsApp, labda huna muunganisho wa intaneti. Ili kuangalia muunganisho wa intaneti wa kifaa chako:
 • Angalia kama kuna aikoni ya saa karibu na ujumbe wako badala ya alama ya tiki. Ikiwa ipo, ina maana kwamba ujumbe wako haujawasilishwa.
 • Angalia ishara ya mtandao kwenye kifaa chako ili uone ikiwa inamweka au haipo.
Utatuaji
Matatizo mengi ya muunganisho yanaweza kusuluhishwa kwa kufanya mojawapo ya yafuatayo:
Mipangilio ya kifaa
 • Anzisha kifaa chako upya kwa kukizima na kukiwasha tena.
 • Sasisha WhatsApp kuwa toleo la karibuni linalopatikana kwenye Duka la Programu la Apple.
 • Fungua Mipangilio
  ya iPhone kisha uwashe na kuzima Hali ya Ndegeni.
 • Fungua Mipangilio
  ya iPhone > gusa Data ya Simu kisha uwashe Data ya Simu.
 • Fungua Mipangilio
  ya iPhone > gusa Wi-Fi kisha uzime na kuwasha Wi-Fi.
 • Boresha au rejesha mfumo wa uendeshaji wa iPhone yako kuwa toleo la hivi karibuni la kifaa chako.
Mipangilio ya Wi-Fi
 • Jaribu kuunganisha kwenye mitandao tofauti ya Wi-Fi.
 • Hakikisha Wi-Fi imewashwa wakati unatumia Sleep Focus.
 • Zima kisha uwashe tena ruta yako ya Wi-Fi.
 • Wasiliana na kampuni inayokupa huduma za simu na uhakikishe mipangilio yako ya APN imewekwa kwa usahihi.
 • Fungua Mipangilio
  ya iPhone > gusa Jumla > Hamisha au Weka Upya iPhone > Weka upya > Weka upya Mipangilio ya Mtandao. Weka namba yako ya siri. Chagua Weka Mipangilio ya Mtandao Upya. (Kufanya hivi kutafuta manenosiri yako yote ya Wi-Fi uliyoyahifadhi).
 • Ukiwa unatatizika kuunganisha kwenye WhatsApp unapotumia mtandao wa Wi-Fi ambao kwa kawaida huwa hauutumii, wasiliana na msimamizi wa mtandao huo.
 • Hakikisha kuwa hutumii mtandao wa Wi-Fi unaodhibitiwa, kama vile ofisini au katika chuo kikuu. Inawezekana kwamba mtandao wako umewekwa mipangilio ili kuzuia au kupunguza miunganisho.
Mipangilio mingine
 • Ikiwa unatumia iPhone ambayo imefunguliwa au SIM kadi unayolipia awali, utahitaji kurekebisha mipangilio ya APN ya kifaa chako ili ifae SIM kadi yako. Wasiliana na kampuni inayokupa huduma za mtandao wa simu kwa maelezo na maelekezo.
 • WhatsApp haijaundwa ili kutumiwa kupitia seva mbadala au huduma za VPN. Mipangilio hiyo haiwezi kutumika.
 • Zima utumiaji wa mtandao wa nje.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La