Kwa nini ninaona ujumbe mpya wa mfumo kwenye soga zangu za WhatsApp?

Tunataka kuweka wazi nini maana ya kuwasiliana na biashara kwenye WhatsApp.
Baadhi ya biashara unazowasiliana nazo kwa soga kwenye WhatsApp zinaweza kuchagua kutumia Facebook au kampuni nyingine kuzisaidia kudhibiti na kuhifadhi ujumbe wao. Biashara ikichagua kutumia huduma za kampuni nyingine kudhibiti ujumbe wake, tutakufahamisha kwa kukuonyesha ujumbe huu wa mfumo:
Ikiwa biashara inadhibiti soga zake kivyake, utaona ujumbe huu wa mfumo:
Hata kama biashara itachagua kutumia Facebook kuweka ujumbe wake, Facebook haitatumia ujumbe wako kiotomatiki kuamua matangazo unayoyaona. Kama ilivyo kwenye njia nyinginezo za mawasiliano -- kama vile vituo vya huduma kwa simu au barua pepe -- biashara zinaweza kutumia mawasiliano na wateja kwa madhumuni yao ya uuzaji, ambayo yanaweza kujumuisha utangazaji kwenye Facebook au kwingineko. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zake za faragha.
Ikiwa hutaki kupokea ujumbe kutoka kwa mtu au biashara, unaweza kumzuia moja kwa moja kwenye soga au umfute kutoka kwenye orodha yako ya anwani.
Salama na faragha wakati wote
Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ile ile ya ufumbaji wa Signal ambayo hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya biashara ya WhatsApp, ujumbe wako huwasilishwa kwa usalama kwenda sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La