Jinsi ya kupiga simu ya video ya kikundi

Kupiga simu ya kikundi huruhusu hadi washiriki wanane kupigiana simu za video kwa kutumia WhatsApp. Unapopokea simu ya video ya kikundi, arifa ya Simu ya video ya kikundi inayoingia au skrini ya simu ya video ya kikundi ya WhatsApp itaonyesha washiriki waliopo kwenye simu na mtu wa kwanza kwenye orodha ndiye mshiriki aliyekuongeza. Unaweza pia kujiunga na simu ambazo hukujibu iwapo bado zinaendelea.
Kupiga simu ya video ya kikundi
Kupiga simu ya video ya kikundi kutoka kwenye soga ya kikundi
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp unachotaka kupigia simu ya video.
 2. Ikiwa kikundi chako cha soga kina washiriki 33 au zaidi, gusa Simu ya kikundi
  .
  • Ikiwa kikundi chako cha soga kina washiriki 32 au wachache, gusa Simu ya video
   kisha uthibitishe uamuzi wako. Watu saba wa kwanza watakaojibu wanaweza kujiunga na simu, ni wanakikundi pekee ndio wanaweza kushiriki.
 3. Tafuta washiriki unaotaka kuwaongeza kwenye simu, kisha gusa Simu ya Video
  .
Kupiga simu ya video ya kikundi kutoka kwenye kichupo cha Simu
 1. Fungua WhatsApp, kisha gusa kichupo cha Simu.
 2. Gusa Simu Mpya
  > Simu Mpya ya Kikundi.
 3. Tafuta washiriki unaotaka kuwaongeza kwenye simu, kisha gusa Simu ya Video
  .
Kupiga simu ya video ya kikundi kutoka kwenye soga ya binafsi
 1. Fungua soga ya WhatsApp iliyo na mmoja wa watu unaotaka kuwapigia simu ya video.
 2. Gusa Simu ya Video
  .
 3. Mara baada ya mshiriki kukubali simu, gusa Fungua
  > Ongeza Mshiriki.
 4. Tafuta mshiriki mwingine unayetaka kumwongeza kwenye simu kisha gusa Ongeza.
 5. Gusa Ongeza Mshiriki
  kama unataka kuongeza washiriki zaidi.
Kujiunga na simu ya video ya kikundi
Kujiunga na simu ya video ya kikundi inayoingia
 1. Utapokea arifa mtu anapokualika ujiunge na simu ya video ya kikundi.
 2. Gusa arifa ili ufungue skrini ya maelezo ya simu.
 3. Kwenye skrini hii, unaweza kukagua kwanza washiriki wa simu na waalikwa wengine.
 4. Gusa Jiunge ili ujiunge na simu.
 5. Ukiwa kwenye simu, gusa Fungua
  ili ufungue skrini ya maelezo ya simu.
  • Gusa Ongeza Mshiriki ili uongeze washiriki zaidi kwenye simu.
  • Gusa Piga ili utume mwaliko kwa watu ambao wameshaalikwa.
Kujiunga na simu ya video ya kikundi ambayo hukujibu
 1. Fungua WhatsApp, kisha gusa kichupo cha SIMU.
 2. Ikiwa simu ilianzishwa kutoka kwenye soga ya kikundi, unaweza kujiunga kwa kufungua soga hiyo halafu uguse Jiunge.
 3. Ikiwa simu inaendelea, gusa simu ambayo ungependa kujiunga nayo. Hatua hii itafungua skrini ya maelezo ya simu.
 4. Gusa Jiunge.
Kumbuka:
 • Ni washiriki wanane tu ndio wanaoweza kuwa katika simu kwa wakati mmoja.
 • Hakikisha kwamba wewe na unaowasiliana nao mna muunganisho imara wa intaneti wakati wa kupiga au kupokea simu za video. Ubora wa simu ya video utategemea mtu mwenye muunganisho hafifu.
 • Wakati wa simu ya video ya kikundi, una chaguo la kuzima video yako kwa kugusa Zima Video
  .
 • Huwezi kuondoa mhusika wakati mko kwenye simu ya video ya kikundi. Mtumiaji atahitaji kukata simu ili kujiondoa kwenye simu hiyo.
 • Ingawa inawezekana kuwa kwenye simu ya video ya kikundi pamoja na mtu uliyemzuia, huwezi kuongeza anwani ambayo umezuia kwenye simu au mtu aliyekuzuia.
Rasilimali zinazohusiana:
 • Jinsi ya kupiga simu ya video kwenye: Android | iPhone
 • Jinsi ya kupiga simu ya video ya kikundi kwenye Android
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La