Jinsi ya kuhamisha akaunti yako ya WhatsApp Messenger kwenda kwenye programu ya WhatsApp Business

Android
iPhone
Kabla ya kuhamisha akaunti yako ya WhatsApp Messenger kwenda kwenye WhatsApp Business, tunapendekeza uunde nakala ya akaunti yako. Pata maelezo ya jinsi ya kuunda nakala kwenye makala haya.
  1. Sasisha WhatsApp Messenger na upakue programu ya WhatsApp Business kutoka kwenye Duka la Programu la Apple.
  2. Fungua programu ya WhatsApp Business.
  3. Soma Masharti ya Huduma ya programu ya WhatsApp Business. Gusa Kubali na Uendelee ili ukubali masharti.
  4. Programu ya WhatsApp Business hutambua kiotomatiki namba unayotumia kwenye WhatsApp Messenger. Ili kuendelea, gusa chaguo lililo na namba yako ya biashara.
  5. WhatsApp itakutumia SMS iliyo na msimbo wenye tarakimu 6. Weka msimbo huo wa tarakimu 6 ili kuthibitisha namba yako.
    • Hutahitaji kukamilisha hatua hii ikiwa unatumia iCloud Keychain na umewahi kuthibitisha namba hii kwenye simu hiyo hiyo hapo awali.
  6. Unda jalada lako la biashara, kisha gusa Nimemaliza.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La