Jinsi ya kuweka upya msimbo wako wa QR wa WhatsApp Business

Kama uliwahi kushiriki msimbo wako wa QR ya WhatsApp lakini hutaki tena mtu yeyote akupate kwa kuichanganua, unaweza kuweka upya msimbo wa QR. Ukiweka msimbo wako wa QR upya, kiungo cha msimbo wako wa awali hautafanya kazi tena. Utahitaji kushiriki tena msimbo mpya wa QR na wateja wako ukichagua kuuweka upya.
Dokezo la Biashara: Unaweza kuweka upya msimbo wako wa QR kwa sababu zozote zile. Ikiwa awali ulishiriki msimbo wako kwenye mitandao ya kijamii lakini umeanza kupokea taka, unaweza kuweka upya msimbo wako ili kuzuia watumaji wasikufikie kwa njia hiyo.
Kuweka upya msimbo wako wa QR
  1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
  2. Gusa Chaguo zaidi
    > Zana za Biashara > Kiungo kifupi.
  3. Gusa Angalia Msimbo wa QR.
  4. Gusa Chaguo zaidi
    > Weka kiungo upya > WEKA UPYA.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La