Vidokezo vya usalama wa akaunti

Unaweza kuweka akaunti yako ya WhatsApp salama kwa kufuata vipengele vifuatavyo:
  • Usishiriki na wengine msimbo wako wa uthibitisho au PIN ya uhakiki wa hatua mbili.
  • Wezesha uhakiki wa hatua mbili na toa anwani ya barua pepe iwapo utasahau PIN yako.
  • Weka msimbo wa kifaa.
  • Kuwa na ufahamu wa anayeweza kufikia simu yako. Kama kuna mtu anayeweza kufikia simu yako, anaweza kutumia akaunti yako ya WhatsApp bila ruhusa yako.
Tunapendekeza ushiriki ushauri huu na marafiki na familia ili kuwasaidia kulinda akaunti zao za WhatsApp.
Dokezo: Ukipokea barua pepe ili ukweke upya PIN ya uhakiki wa hatua mbili, lakini haukuiomba, usibofye kwenye kiungo. Mtu fulani anaweza kuwa anajaribu kuhakiki namba yako ya simu kwenye WhatsApp.
Rasilimali
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La