Jinsi ya kushiriki bidhaa au huduma na wateja

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Android
iPhone
Unaweza kushiriki bidhaa na huduma zako na wateja wapya na waliopo kwa kushiriki katalogi yako.
Kushiriki katalogi yako kwenye soga ya binafsi au soga ya kikundi
 1. Fungua soga kwenye programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa Ambatisha
  kando ya sehemu ya maandishi. Kisha, gusa Katalogi.
 3. Gusa Tuma
  .
Kushiriki bidhaa au huduma kwenye soga ya binafsi au soga ya kikundi
 1. Fungua soga kwenye programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa Ambatisha
  kando ya sehemu ya maandishi. Kisha, gusa Katalogi.
 3. Teua bidhaa au huduma unayopenda kushiriki.
 4. Gusa Tuma
  .
Kushiriki katalogi nzima
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Zana za biashara > Katalogi.
 3. Gusa Chaguo zaidi > Shiriki.
 4. Kisha unaweza kutuma kiungo kwa watu walio kwenye anwani zako au wateja watarajiwa kupitia programu ya WhatsApp Business au ushiriki kiungo kupitia barua pepe au programu nyingine za kutuma ujumbe.
Kushiriki bidhaa au huduma mahususi
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
 2. Teua bidhaa au huduma unayopenda kushiriki.
 3. Gusa Chaguo zaidi.
 4. Kisha unaweza kusambaza au kushiriki bidhaa au huduma mahususi na walio kwenye anwani zako au wanunuzi watarajiwa kwa kuchagua hiari zifuatazo:
  • Sambaza bidhaa
   : Kushiriki bidhaa moja kwa moja na walio kwenye anwani zako kupitia kwenye programu ya WhatsApp Business.
  • Shiriki
   : Kushiriki kiungo cha bidhaa kupitia programu ya WhatsApp Business, barua pepe au programu nyingine za kutuma ujumbe.
Kumbuka: Katalogi na viungo vya bidhaa haviwezi kubadilishwa kabla ya kushirikiwa kwa sababu vinatolewa kiotomatiki.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La