Jinsi ya kutumia majibu ya haraka

Kwa majibu ya haraka, unaweza kuunda njia za mkato za ujumbe unaotuma kwa wateja wako mara kwa mara. Hili linaweza kujumuisha ujumbe wa maudhui, kama vile picha na video.
Kumbuka: Unaweza kuhifadhi hadi majibu 50 ya haraka.
Kuweka majibu ya haraka
 1. Kwenye programu ya WhatsApp Business, gusa Chaguo zaidi
  > Zana za biashara > Majibu ya haraka.
 2. Gusa Ongeza
  .
 3. Gusa Tuma ujumbe ili utunge ujumbe unaoutaka.
  • Kumbuka: Faili za maudhui hazitumiki katika majibu ya haraka kwenye matoleo ya Web au Desktop.
 4. Gusa Njiamkato ili uweke njiamkato ya kibodi kwa ajili ya majibu yako ya haraka.
 5. Gusa HIFADHI.
Majibu chaguomsingi
Ili kurahisisha kuwasiliana na wateja wako, programu ya WhatsApp Business huleta majibu ya haraka kulingana na taarifa zilizo kwenye jalada lako la biashara. Unaweza kutuma jibu la haraka lililo na saa zako za kazi, anwani yako au hata jalada lako lenyewe. Ili uone majibu haya chaguomsingi:
 • Fungua soga, gusa Tuma ujumbe kisha andika "/" au
 • Fungua soga, gusa Ambatisha
  > Majibu ya Haraka.
Kutumia majibu ya haraka
Kama kiambatisho
 1. Fungua soga.
 2. Gusa Ambatisha
  > Majibu ya Haraka.
 3. Chagua jibu la haraka unalopendelea. Ujumbe utaonekana kiotomatiki katika sehemu ya kuandikia.
 4. Hariri ujumbe au gusa tu Tuma
  .
Kutoka katika sehemu ya maandishi
 1. Fungua soga.
 2. Gusa Tuma ujumbe, kisha andika "/". Kufanya hivyo kutaleta majibu yako yote ya haraka, ikiwa ni pamoja na majibu chaguomsingi.
 3. Chagua jibu la haraka unalopendelea. Ujumbe utaonekana kiotomatiki katika sehemu ya kuandikia.
 4. Hariri ujumbe au gusa tu Tuma
  .
Kidokezo cha Kibiashara: Kumbuka kujaza kila sehemu katika jalada lako la biashara ili upate majibu chaguomsingi ambayo unaweza kuyatumia kuwajulisha wateja kuhusu anwani, saa zako za kazi na zaidi.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La