Jinsi ya kuunda na kualika washiriki kwenye kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kuunda kikundi cha WhatsApp chenye hadi washiriki 256.
Kuunda kikundi
 1. Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
  > Kikundi kipya.
  • Au, gusa Soga mpya
   > Kikundi kipya.
 2. Tafuta au chagua watumiaji unaotaka kuwaweka kwenye kikundi. Kisha, gusa aikoni ya kishale cha kijani.
 3. Weka mada ya kikundi. Hili litakuwa jina la kikundi ambalo washiriki wote wataliona.
  • Ukomo wa mada ni herufi 25.
  • Unaweza kugusa Emoji
   ili uweke emoji kwenye mada yako.
  • Unaweza kuweka aikoni ya kikundi kwa kugusa aikoni ya Kamera. Unaweza kuchagua kutumia Kamera, Matunzio au Tafuta Mtandaoni ili uongeze picha. Ukishaweka, aikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye kichupo cha SOGA.
 4. Gusa aikoni ya tiki ya kijani unapomaliza.
Kualika watu kwenye vikundi kupitia viungo
Ukiwa msimamizi wa kikundi, unaweza kuwaalika watu wajiunge na kikundi kwa kushiriki nao kiungo. Msimamizi anaweza Kubadilisha kiungo wakati wowote ili kubatilisha kiungo cha mwaliko wa awali na kuunda kiungo kipya.
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Chaguo zaidi
   > Maelezo ya kikundi.
 2. Gusa Alika kupitia kiungo.
 3. Chagua Kutuma kiungo kupitia WhatsApp, Nakili kiungo, Shiriki kiungo kupitia programu nyingine au msimbo wa QR.
  • Kama unatuma kupitia WhatsApp, tafuta au chagua mtumiaji, kisha gusa Tuma
   .
  • Ili ubadilishe kiungo, gusa Weka kiungo upya > WEKA KIUNGO UPYA.
Kumbuka:
 • Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unayemtumia kiungo cha mwaliko anaweza kujiunga na kikundi, kwa hivyo tumia kipengele hiki tu kwa watu unaowaamini. Inawezekana kwa mtu kusambaza kiungo kwa watu wengine, ambao wanaweza kujiunga na kikundi bila ruhusa ya ziada kutoka kwa msimamizi wa kikundi.
 • Tunaongeza ukubwa wa vikundi hatua kwa hatua katika miezi ijayo na huenda kukawa na kuchelewa kufikia kipengele hiki.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La