Jinsi ya kunyamazisha au kuruhusu arifa za kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kunyamazisha arifa za kikundi kwa muda maalum. Bado utapokea ujumbe uliotumwa kwenye soga ya kikundi, lakini simu yako haitatetema au kutoa sauti ujumbe unapopokelewa. Ujumbe unaotumwa kwenye soga zilizonyamazishwa hautaonyeshwa kwenye idadi ya beji katika aikoni ya WhatsApp isipokuwa kama umetajwa au kujibiwa kwenye soga.
Kunyamazisha arifa za kikundi
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha, gusa Zaidi
   > Nyamazisha.
 2. Gusa Nyamazisha
  .
 3. Chagua muda ambao ungependa kunyamazisha arifa.
Kurejesha arifa za kikundi
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha gusa Zaidi
   > Rejesha arifa.
 2. Gusa Iliyonyamazishwa
  .
 3. Gusa Rejesha arifa.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La