Jinsi ya kutumia ujumbe wa kutokuwepo

Ukiwasha kipengele cha ujumbe wa kutokuwepo, wateja ambao watakutumia ujumbe watapokea kiotomatiki ujumbe unaoweza kubadilisha, ukiwaambia kuwa una shughuli au upo mbali na simu yako. Unaweza kuchagua ni wateja gani utawatumia ujumbe wa kutokuwepo na ujumbe utumwe lini.
Dokezo la Kibiashara: Kutumia ujumbe wa kutokuwepo hakukusaidii tu kuwa na muda wako wa binafsi. Pia kunawahakikishia wateja wako kuwa hujawapuuza.
Kuweka ujumbe wa kutokuwepo
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa Mipangilio > Zana za biashara > Ujumbe wa kutokuwepo.
 3. Washa Tuma ujumbe wa kutokuwepo.
 4. Chini ya Ujumbe, gusa ujumbe huo ili kuuhariri, kisha gusa Hifadhi.
 5. Gusa Ratiba ili kuratibu ujumbe wako wa kutokuwepo. Chagua miongoni mwa zifuatazo:
  • Tuma kila wakati: Ili utume kila wakati.
  • Ratiba binafsi: ili utume tu wakati maalum.
  • Nje ya saa za kazi: ili utume tu nje ya saa za kazi.
   • Kumbuka: Chaguo hili linapatikana tu ikiwa umeweka saa zako za kazi kwenye jalada lako la biashara.
 6. Gusa Wapokeaji ili kuamua ni nani atapokea ujumbe wako wa kutokuwepo. Chagua miongoni mwa zifuatazo:
  • Kila mtu: kutuma ujumbe kwa yeyote anayekutumia ujumbe wakati kipengele cha Ujumbe wa Kutokuwepo kimewashwa.
  • Kila mtu asiye kwenye kitabu cha anwani: kutuma tu kwa wateja ambao hawapo kwenye kitabu chako cha anwani.
  • Kila mtu isipokuwa…: kutuma kwa wateja wote isipokuwa wale uliowachagua.
  • Tuma tu kwa…: kutuma tu kwa watu unaowachagua.
Kumbuka: Lazima kifaa chako kiwe na muunganisho wa intaneti ili kutuma ujumbe wa kutokuwepo.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La