Jinsi ya kuwasha au kuzima ujumbe unaotoweka kwenye kikundi

Unaweza kutuma ujumbe unaotoweka kwenye WhatsApp kwa kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka. Unaweza kuchagua ujumbe utoweke baada ya saa 24, siku 7 au siku 90. Mara baada ya kuwashwa, ujumbe mpya unaotumwa kwenye soga utatoweka baada ya kipindi cha muda ulichochagua. Ujumbe uliotumwa au kupokelewa kabla ya kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka hautaathiriwa.
Kuwasha ujumbe unaotoweka
Kwenye soga ya kikundi, washiriki wowote wa kikundi wanaweza kuwasha ujumbe unaotoweka. Hata hivyo, msimamizi wa kikundi anaweza kubadilisha mipangilio ya kikundi ili kuruhusu wasimamizi tu kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio ya usimamizi wa kikundi katika makala haya.
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp.
 2. Bonyeza Chaguo > Maelezo ya kikundi > SAWA.
 3. Teua Ujumbe unaotoweka > HARIRI.
  • Ukiulizwa, bonyeza Inayofuata > SAWA.
 4. Chagua Saa 24, Siku 7 au Siku 90 > SAWA.
Pia unaweza kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka wakati unaanzisha soga mpya ya kikundi.
Kuzima ujumbe unaotoweka
Mtu yeyote katika soga ya kikundi anaweza kuzima ujumbe unaotoweka wakati wowote, isipokuwa kama msimamizi wa kikundi amewaachia wasimamizi pekee uwezo huo.
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp.
 2. Bonyeza Chaguo > Maelezo ya kikundi > SAWA.
 3. Teua Ujumbe unaotoweka > HARIRI.
  • Ukiulizwa, bonyeza Inayofuata > SAWA.
 4. Chagua Zima > SAWA.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La