Jinsi ya kufuta ujumbe

Unaweza kufuta ujumbe kwako mwenyewe au kuomba ujumbe ufutwe kwa kila mtu.
Kufuta ujumbe kwa kila mtu
Kufuta ujumbe kwa kila mtu hukuruhusu ufute ujumbe mahususi uliotuma kwenye soga ya binafsi au ya kikundi. Hii ni muhimu hasa ikiwa ulituma ujumbe kwenye soga isiyo sahihi au kama ujumbe uliotuma una makosa.
Ujumbe ambao umefutwa kwa kila mtu utawakilishwa na:
Ujumbe huu ulifutwa
Kufuta ujumbe kwa kila mtu:
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kuufuta.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe husika > chagua Futa kwenye menyu. Ukipenda, chagua ujumbe zaidi ili kufuta ujumbe kadhaa kwa wakati mmoja.
  • Ukiulizwa, gusa Zaidi
   > chagua Futa kwenye menyu.
 3. Gusa Futa
  > Futa kwa Kila Mtu.
Kumbuka:
 • Ili ujumbe ufutwe kwa kila mtu, wewe na wapokeaji lazima muwe mnatumia toleo la karibuni la WhatsApp.
 • Wapokeaji wanaotumia toleo la WhatsApp la iOS bado wanaweza kuwa na maudhui uliyotuma yakiwa yamehifadhiwa kwenye Picha zao, hata baada ya kufutwa kwenye soga ya WhatsApp.
 • Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla haujafutwa au kama ufutaji haukukamilika.
 • Hutaarifiwa kama ufutaji haukufanikiwa kwa kila mtu.
 • Una kama saa moja tu baada ya kutuma ujumbe kuomba Kufuta kwa Kila Mtu.
Kujifutia ujumbe
Unaweza kufuta nakala ya ujumbe wako uliotuma au kupokea kwenye simu yako. Hatua hii haina athari kwa soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona ujumbe katika skrini zao za soga.
Kujifutia ujumbe:
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kuufuta.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe husika > chagua Futa kwenye menyu. Ukipenda, chagua ujumbe zaidi ili kufuta ujumbe kadhaa kwa wakati mmoja.
  • Ukiulizwa, gusa Zaidi
   > chagua Futa kwenye menyu.
 3. Gusa Futa
  > Futa Kwangu.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kufuta ujumbe: Android | KaiOS
Jinsi ya kuondoa soga: Android | iPhone
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La