Jinsi ya kuongeza na kuondoa washiriki

Unaweza kuongeza au kuwaondoa washiriki kwenye kikundi ikiwa wewe ndiwe msimamizi wa kikundi.
Kuongeza washiriki
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Chaguo zaidi
   > maelezo ya kikundi.
 2. Gusa Ongeza washiriki
  .
 3. Tafuta au chagua waasiliani wa kuongeza kwenye kikundi.
 4. Gusa alama hakikishi ya kijani
  unapomaliza.
Kuondoa washiriki
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Chaguo zaidi
   > maelezo ya kikundi.
 2. Gusa mshiriki unayetaka kumwondoa.
 3. Gusa Ondoa {participant} > SAWA.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La