Kuhusu kuhifadhi hati za utambulisho wa WhatsApp katika kifunguo cha iCloud

iPhone
Unaposajili namba ya simu kwenye programu ya WhatsApp Messenger au WhatsApp Business, utapokea msimbo wa tarakimu-6 kuthibitisha namba hiyo ya simu. Ikiwezeshwa, Kifungua cha iCloud kinahifadhi hati zako za utambulisho, kukuruhusu kusajili namba yako kwa kifaa kipya bila kupitia mchakato wa uthibitisho.
Kumbuka: Kusajili namba mpya ya simu itahitaji uthibitisho wa SMS hata kama Kifunguo cha iCloud kimewezeshwa.
Maelezo yote yaliyohifadhiwa kwenye Kifunguo cha iCloud yamefumbwa mwisho-kwa-mwisho. Apple wala WhatsApp haziwezi kufikia maelezo hayo.
Wasiliana na msaada wa Apple ili kujifunza zaidi kuhusu Kifunguo cha iCloud na jinsi ya kukiwezesha.
Rasilimali
Kujifunza zaidi kuhusu kuthibitisha namba yako ya simu kwenye iPhone, soma makala hii.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La