Kuhusu vifaa vinavyoweza kutumika

Android
iPhone
Mfumo wetu unaweza kutumika kwenye vifaa vya Android ambavyo vinakidhi matakwa yafuatayo:
  • Simu yako ya Android inatumia mfumo wa uendeshaji wa toleo la OS 4.1 au matoleo ya baadaye.
  • Simu yako ya Android inaweza kupokea SMS au simu wakati wa mchakato wa uthibitishaji.
Kumbuka: Kuanzia tarehe 24 Oktoba, 2023, toleo la Android OS 5.0 na matoleo mapya zaidi ndio yatakayotumika.
Maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyochagua ni mifumo ipi ya uendeshaji tunaweza kuitumia na kinachotokea ikiwa mfumo wako hautaendelea kutumika yanapatikana hapa.
Ili kuendana na maendeleo ya hivi punde zaidi kwenye teknolojia, mara kwa mara huwa tunaacha kutumia mifumo ya uendeshaji ya zamani ili kuelekeza juhudi zetu katika kufanikisha mifumo mipya zaidi.
Ikiwa tutaacha kutoa huduma kwa mfumo wako wa uendeshaji, utaarifiwa na kukumbushwa mara kadhaa ili upate kifaa kipya na uendelee kutumia WhatsApp. Pia tutasasisha ukurasa huu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa toleo jipya zaidi la Android linalotumika kwenye mfumo wetu limeorodheshwa hapa.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La