Jinsi ya kuhamisha akaunti yako ya WhatsApp Messenger kwenda kwenye programu ya WhatsApp Business

Kabla ya kuhamisha akaunti yako ya WhatsApp Messenger kwenda kwenye WhatsApp Business, tunapendekeza uunde nakala ya akaunti yako. Pata maelezo ya jinsi ya kuunda nakala kwenye makala haya.
  1. Sasisha WhatsApp Messenger na upakue WhatsApp Business kutoka kwenye Duka la Google Play.
  2. Fungua programu ya WhatsApp Business.
  3. Soma Masharti ya Huduma ya programu ya WhatsApp Business. Gusa KUBALI NA UENDELEE ili ukubali masharti.
  4. Programu ya WhatsApp Business hutambua kiotomatiki namba unayotumia kwenye WhatsApp Messenger. Ili kuendelea, gusa chaguo lililo na namba yako ya biashara.
  5. Gusa ENDELEA > RUHUSU ili uruhusu programu ya WhatsApp Business ifikie historia ya soga na maudhui.
  6. WhatsApp itakutumia SMS iliyo na msimbo wenye tarakimu 6. Weka msimbo huo wa tarakimu 6 ili kuthibitisha namba yako.
  7. Unda jalada lako la biashara, kisha gusa INAYOFUATA.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La