Jinsi ya kufuta akaunti yako

Android
iPhone
KaiOS
Unaweza kufuta akaunti yako ndani ya WhatsApp. Kufuta akaunti yako ni mchakato usioweza kutenduliwa, hatuwezi kuubatilisha hata kama umeufanya kimakosa.
Kufuta akaunti yako:
 1. Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Akaunti > Futa akaunti yangu.
 2. Chagua msimbo wa nchi yako kisha uweke nambari yako ya simu.
 3. Bonyeza Futa > FUTA.
Kufuta akaunti yako kutafanya yafuatayo:
 • Kutafuta akaunti yako kutoka kwenye WhatsApp.
 • Kutafuta historia ya soga zako kwenye simu yako.
 • Kutakufuta kutoka kwenye vikundi vyote vya WhatsApp.
Ukiifuta akaunti yako:
 • Huwezi kurejesha upatikanaji wa akaunti yako.
 • Inaweza kuchukua hadi siku 90 kutoka mwanzo wa mchakato wa kufuta ili kufuta taarifa zako zilizo kwenye WhatsApp. Nakala ya taarifa zako huenda pia zikabaki baada ya siku 90 kwenye hifadhi ya nakala ambayo huwa tunaitumia ili kurejesha taarifa endapo kuna mkasa, hitilafu ya programu au tukio jingine la kupoteza data. Hutapata taarifa zako kwenye WhatsApp katika kipindi hicho.
 • Hutaathiri taarifa zako zinazohusiana na vikundi ulivyounda au taarifa ambazo watumiaji wengine wanazo zinazohusiana na wewe, kama vile nakala za ujumbe uliowatumia.
 • Tunaweza kubaki na kiasi cha data ya kumbukumbu kwenye hifadhidata yetu hata ukishafuta akaunti yako, lakini data kama hiyo haitakuwa na taarifa yoyote inayotambulisha kiasi kwamba haiwezi tena kuhusishwa na akaunti yako. Ili kufanya hivi, mara kwa mara, tunafuta taarifa fulani tambulishi kutoka kwenye data hii ya kumbukumbu na tunabadilisha matukio yoyote ya kitambulisho cha akaunti yako na kuweka kitambulisho mbadala ambacho hakiwezi kuhusishwa tena na akaunti yako mara tu inapofutwa.
 • Pia tunaweza kuhifadhi taarifa zako kwa ajili ya mambo kama vile, masuala ya kisheria, ukiukaji wa masharti au juhudi za kuzuia madhara.
 • Tafadhali rejelea Sera yetu ya Faragha kwa taarifa zaidi.
 • Taarifa yako uliyoshiriki na Kampuni zingine za Meta pia itafutwa.
Rasilimali zinazohusiana:
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufuta akaunti yako kwenye: Android | iPhone
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La