Â
Jinsi ya kufuta akaunti yako
Android
iPhone
KaiOS
Unaweza kuifuta akaunti yako ndani ya WhatsApp. Kufuta akaunti yako ni mchakato usioweza kutenduliwa, ambao hatuwezi kuubatilisha hata kama umeufanya kimakosa.
Kuifuta akaunti yako
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Chaguo zaidi> Mipangilio > Akaunti > Futa akaunti yangu.
- Weka nambari yako ya simu katika mfumo kamili wa kimataifa kisha uguse FUTA AKAUNTI YANGU.
- Chagua sababu ya kufuta akaunti kutoka kwenye orodha kujunzi.
- Gusa FUTA AKAUNTI YANGU.
Kufuta akaunti yako kutafanya yafuatayo:
- Kutafuta akaunti yako kutoka kwa WhatsApp.
- Kutafuta historia yako ya ujumbe.
- Kutakufuta kutoka kwenye vikundi vyako vyote vya WhatsApp.
- Kutafuta nakala uliyoweka kwenye Hifadhi ya Google.
Ukiifuta akaunti yako:
- Huwezi kurejesha upatikanaji wa akaunti yako.
- Inaweza kuchukua hadi siku 90 kutoka mwanzo wa mchakato wa kufuta ili kufuta taarifa zako zilizo kwenye WhatsApp. Nakala ya taarifa zako huenda pia zikabaki baada ya siku 90 kwenye hifadhi ya nakala ambayo huwa tunaitumia ili kurejesha taarifa endapo kuna mkasa, hitilafu ya programu au tukio jingine la kupoteza data. Hutapata taarifa zako kwenye WhatsApp katika kipindi hicho.
- Hutaathiri taarifa zako zinazohusiana na vikundi ulivyounda au taarifa ambazo watumiaji wengine wanazo zinazohusiana na wewe, kama vile nakala za ujumbe uliowatumia.
- Tunaweza kubaki na kiasi cha data ya kumbukumbu kwenye hifadhidata yetu hata ukishafuta akaunti yako, lakini data kama hiyo haitakuwa na taarifa yoyote inayotambulisha kiasi kwamba haiwezi tena kuhusishwa na akaunti yako. Ili kufanya hivi, mara kwa mara, tunafuta taarifa fulani tambulishi kutoka kwenye data hii ya kumbukumbu na tunabadilisha matukio yoyote ya kitambulisho cha akaunti yako na kuweka kitambulisho mbadala ambacho hakiwezi kuhusishwa tena na akaunti yako mara tu inapofutwa.
- Pia tunaweza kuhifadhi taarifa zako kwa ajili ya mambo kama vile, masuala ya kisheria, ukiukaji wa masharti au juhudi za kuzuia madhara.
- Tafadhali rejelea Sera yetu ya Faragha kwa taarifa zaidi.
- Taarifa yako uliyoshiriki na Kampuni zingine za Meta pia itafutwa.
Rasilimali zinazohusiana: