Â
Jinsi ya kuripoti katalogi au biashara
Android
iPhone
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Ikiwa unaamini kuwa biashara inakiuka Sera yetu ya Uuzaji, unaweza kuiripoti.
Kuripoti huduma au bidhaa
- Fungua soga kati yako na biashara hiyo.
- Gusa jina la biashara.
- Karibu na Katalogi, gusa TAZAMA ZOTE.
- Gusa bidhaa au huduma.
- Gusa Zaidi> Ripoti.
- Una machaguo mawili:
- Kuripoti bidhaa au huduma, gusa Ripoti.
- Ili utoe maelezo zaidi, gusa Tuambie Zaidi, kisha uteue chaguo kisha uguse Wasilisha.
Kuripoti biashara
- Nenda kwenye jalada la WhatsApp Business kisha usogeze hadi chini.
- Gusa Ripoti Biashara.
- Una machaguo mawili:
- Kuzuia na kuripoti biashara, gusa kisanduku cha kuteua karibu na Zuia biashara na ufute soga. Kisha, uguse Ripoti.
- Ili uripoti biashara, gusa Ripoti.