Jinsi ya kutuma na kufungua maudhui ya kutazama mara moja

Unaweza kutuma picha au video ambayo itatoweka kwenye WhatsApp baada ya mpokeaji kuifungua na kufunga sehemu ya kuangalilia maudhui. Mara tu akishafunga sehemu ya kuangalilia maudhui, maudhui hayo hayataonekana tena kwenye soga hiyo na hayawezi kutazamwa tena. Picha au video za kutazamwa mara moja haziwezi kuhifadhiwa kwenye Picha au Matunzio ya mpokeaji na hawezi kuzisambaza.
Kutuma maudhui ya kutazama mara moja
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Bofya +.
 3. Chagua unachotaka kutuma, kisha bonyeza:
  • Picha ili kupiga picha au video mpya kwa kamera yako au kuchagua picha iliyopo kutoka kwenye maktaba yako.
  • Video ili kurekodi video mpya kwa kamera yako au kuchagua video iliyopo kwenye simu yako.
 4. Bonyeza Chagua > Chaguo, kisha chagua Kutazama mara moja.
 5. Bonyeza TUMA.
Utaona arifa ya kuwa Imefunguliwa kwenye soga mara baada ya mpokeaji kutazama picha au video hiyo.
Kufungua maudhui ya kutazama mara moja
 1. Fungua ujumbe wenye 1
  .
 2. Tazama picha au video.
Utaona arifa ya Imefunguliwa kwenye soga kwa maudhui ambayo tayari umeyatazama. Mara baada ya kufunga sehemu ya kuangalilia maudhui, huwezi kutazama maudhui hayo tena au kuripoti maudhui hayo kwa WhatsApp na hayatahifadhiwa kwenye gombo la kamera yako.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La