Haiwezi kupakua au kutuma faili za media

Kama una tatizo kupakua au kutuma picha, video na ujumbe wa sauti, angalia yafuatayo:
  • Simu yako ina upatikanaji wa intaneti kamili na ishara yenye nguvu. Jaribu kupakia ukurasa wa tovuti ili kuhakikisha.
  • Tarehe na wakati wa simu yako ni sahihi. Ikiwa tarehe yako si sahihi, hutaweza kujiunga kwenye seva za WhatsApp kupakua media yako. Jifunze jinsi ya kuweka tarehe yako kwa usahihi hapa.
Kama tatizo linaendelea, inawezekana kuna shida kwenye SD kadi yako. Kuhakiki, hakikisha kadi yako ya SD ina:
  • Nafasi ya kutosha ya hifadhi. Ikiwa kuna nafasi ya kutosha kwenye kadi ya SD, lakini bado huwezi kupakua faili lolote kutoka kwa WhatsApp, huenda unahitaji kufuta data ya WhatsApp kutoka kwenye kadi yako ya SD.
  • Hali ya kusoma tu imezimwa.
Kama hakuna suluhisho la tatizo hili, inamaanisha kuwa kadi yako kadi ya SD imeharibika. Kama ni hivyo, inawezekana unahitaji kuumbiza upya kadi yako ya SD au kununua SD kadi ya SD mpya.
Dondoo: Kuumbiza upya kadi ya SD kutafuta maudhui yote kwenye kadi ya SD.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La