Jinsi ya kutumia hali ya giza

Android
iPhone
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Hali nyeusi inakuruhusu kubadilisha rangi ya mandhari ya WhatsApp kutoka nyeupe kuwa nyeusi na unaweza kuiwasha au kuizima kwenye mipangilio ya kifaa chako au Kituo cha Udhibiti. Kipengele hiki kinapatikana kwenye iOS 13 na matoleo ya baadaye.
Kuwasha hali nyeusi kutoka kwenye mipangilio ya kifaa chako
 1. Nenda kwenye Mipangilio ya iPhone > Mwonekano na Ung'avu.
 2. Chagua kati ya zifuatazo chini ya MWONEKANO:
  • Nyeusi: Kuwasha hali nyeusi.
  • Mwanga: Kuzima hali nyeusi.
  • Otomatiki: Kuwasha hali nyeusi kiotomatiki wakati fulani maalumu. Gusa Chaguo kisha chagua Machweo hadi Mawio au weka Ratiba Maalumu.
Kuwasha hali nyeusi kutoka kwenye Kituo cha Udhibiti
 1. Nenda kwenye Mipangilio ya iPhone > Kituo cha Udhibiti.
 2. Ongeza Hali Nyeusi chini ya UDHIBITI ULIOJUMUISHWA ili ionekane kwenye Kituo cha Udhibiti.
 3. Fungua Kituo cha Udhibiti:
  • Kwenye iPhone X na mpya zaidi, telezesha chini kutokea juu upande wa kulia mwa skrini.
  • Kwenye iPhone 8 na za zamani, telezesha juu kutoka chini ya skrini.
 4. Gusa aikoni ya hali nyeusi ili kuwasha au kuzima hali nyeusi.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La