Haiwezi kupokea arifa kwenye Firefox

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Ikiwa hupokei arifa kwenye WhatsApp Web, hakikisha umewasha upokeaji wa arifa kwenye kivinjari chako.
Kuwasha arifa
  1. Kwenye kivinjari chako, bofya Washa arifa kwenye eneokazi, fanya hivyo kwenye bendera ya bluu juu ya orodha yako ya soga.
  2. Fuata maagizo kwenye skrini.
Kumbuka: Ikiwa huoni bendera ya bluu, pakia ukurasa upya. Ikiwa bado huoni bendera, huenda umesitisha au umezima arifa kwenye mipangilio yako ya WhatsApp.
Kuruhusu arifa
  1. Kwenye kivinjari chako, bofya aikoni ya Menyu, kisha bofya Chaguo au Mapendeleo.
  2. Bofya Faragha na Usalama.
  3. Chini ya Ruhusa, bofya Mipangilio… karibu na Arifa.
  4. Kama menyu kunjuzi ya "web.whatsapp.com" imewekwa kwenye Zuia, ibadilishe iwe Ruhusu.
  5. Bofya Hifadhi Mabadiliko.
Au, bofya aikoni ya kufuli karibu na "https://web.whatsapp.com/". Kama Tuma Arifa inaonyesha ikiwa Imezuiwa, bofya "x", kisha upakie ukurasa upya.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La