Jinsi ya kupiga simu ya video

Android
iPhone
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Simu ya video hukuruhusu kuwapigia watu unaowasiliana nao simu bila malipo kwa kutumia WhatsApp Desktop, hata kama wapo nchi nyingine. Simu ya video hutumia muunganisho wako wa intaneti. Unaweza kupiga simu kwenye kompyuta inayotumia mfumo wa Windows 10 64-bit toleo la 1903 au matoleo ya baadaye na toleo la macOS 10.13 au matoleo ya baadaye. Bado haiwezekani kupiga simu za vikundi kwenye WhatsApp Desktop kwa wakati huu.
Kupiga simu kupitia kompyuta
Ili upige au upokee simu za video kwenye WhatsApp Desktop:
 • Utahitaji muunganisho wa intaneti unaofanya kazi kwenye kompyuta na simu yako.
 • WhatsApp inahitaji kufikia maikrofoni na kamera ya kompyuta yako.
 • Utahitaji kuwa na kifaa cha kutoa sauti, maikrofoni, na kamera iliyounganishwa kwenye kompyuta yako kwa ajili ya simu. Huwezi kupiga simu ya video kwenye kifaa ambacho hakina kamera.
Kumbuka: Tumia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani kwa sauti bora. Kutumia vifaa tofauti kwa ajili ya maikrofoni na spika kunaweza kusababisha mwangwi.
Kupiga simu ya video
 1. Fungua soga ya binafsi na mtumiaji unayetaka kumpigia simu.
 2. Bofya aikoni ya Simu ya video.
Wakati wa simu, unaweza kuzima au kuwasha maikrofoni yako kwa kubofya aikoni ya Maikrofoni au kuzima au kuwasha kamera yako kwa kubofya aikoni ya Kamera. Ili ukate simu, bofya Kata simu.
Kupokea simu ya video
Ikiwa kuna simu inayoingia, unaweza kubofya:
 • Kubali ili upokee simu.
 • Kataa ili ukate simu.
 • Puuza au x ili upuuze simu.
Kubadilisha kati ya simu ya sauti na simu ya video
Ukiwa kwenye simu ya sauti na mtu unayewasiliana naye, unaweza kuomba kubadilisha ili mtumie simu ya video. Mtu unayempigia simu anaweza kubofya Sawa au Badilisha ili kubadilisha simu au Ghairi ili kukata.
 1. Wekelea kiashiria kwenye aikoni ya Kamera wakati wa simu.
 2. Bofya aikoni ya Kamera.
 3. Simu ya sauti itabadilika kuwa simu ya video ikiwa unayewasiliana naye atakubali kubadilisha.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La