Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp hukuruhusu kuwasiliana papo hapo na watu pamoja na vikundi. Unaweza kuutumia kuwasilisha taarifa muhimu na za haraka. Kwa hivyo, ujumbe wote wa sauti hupakuliwa kiotomatiki.
Kutuma ujumbe wa sauti
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Gusa na ushikilie maikrofoni
  na uanze kuzungumza.
 3. Mara unapomaliza, ondoa kidole chako kwenye maikrofoni
  . Ujumbe wa sauti utatumwa kiotomatiki.
Wakati unarekodi ujumbe wa sauti, unaweza kutelezesha kidole ili kughairi
.
Kurekodi ujumbe mrefu wa sauti
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Gusa na ushikilie maikrofoni
  halafu uanze kuzungumza.
 3. Telezesha kidole juu ili uanze kurekodi bila kushikilia.
 4. Mara unapomaliza, gusa Tuma
  ili utume ujumbe.
Wakati unarekodi ujumbe mrefu wa sauti, unaweza kugusa Ghairi ili ughairi. Unaweza pia kugusa kitufe chekundu cha kusitisha
ili usitishe kunakili au uhakiki rasimu ya ujumbe wako. Gusa aikoni nyekundu ya maikrofoni
ili kuendelea kunakili kwenye ujumbe huo huo wa sauti.
Kumbuka: Kwenye baadhi ya simu, huenda itakubidi usubiri kwa sekunde kabla ya kuzungumza ikiwa mwanzo wa ujumbe wako haukurekodiwa.
Kwenye ujumbe wa sauti uliotumwa utaona:
 • Maikrofoni ya kijivu
  kwa ujumbe wa sauti ambao haujachezwa na wapokeaji wote (lakini unaweza kuwa umechezwa na baadhi).
 • Maikrofoni ya bluu
  kwa ujumbe wa sauti ambao wapokeaji wote wameucheza.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La