Jinsi ya kusasisha programu ya Biashara ya WhatsApp.

Unaweza kusasisha programu ya Biashara ya WhatsApp kwenye duka la programu la kifaa chako.
Tunakuhimiza utumie toleo jipya la WhatsApp kila wakati. Matoleo mapya yana vipengele vipya zaidi na marekebisho ya hitilafu.
Android
Tafuta programu ya Biashara ya WhatsApp kwenye Duka la Google Play, kisha udonoe Sasisha.
iPhone
Tafuta programu ya Biashara ya WhatsApp kwenye Apple App Store, kisha udonoe SASISHA.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La