Jinsi ya kusimamia milio ya mazungumzo

Android
Milio ya mazungumzo ni sauti zinazochezwa unapotuma na kupokea ujumbe. Kwa kawaida, milio ya mazungumzo yako yamewashwa. Kiwango cha milio ya mazungumzo kinasimamiwa na kiwango cha arifa za simu yako.
Kuzima au kuwasha milio hii:
  1. Fungua WhatsApp.
  2. Gusa Hiari zaidi
    > Mipangilio > Arifa > zima/washa Milio ya mazungumzo.
Tafadhali zingatia kuwa kurekebisha milio ya mazungumzo kutarekebisha milio ya jumbe zinazoingia na kutoka.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La