Imeshindwa kuunda au kurejesha nakala iliyo katika Hifadhi ya Google

Ikiwa WhatsApp haitambui nakala, inaweza kuwa ni kwa sababu:
 • Hujaingia katika akaunti ile ile ya Google.
 • Hutumii nambari ile ile ya simu uliyotumia kuunda nakala.
 • Kadi yako ya SD au historia ya soga zako imevurugika.
 • Faili la nakala haipo kwenye akaunti ya Hifadhi ya Google au ndani ya kifaa chako.
Imeshindwa kuunda nakala kwenye Hifadhi ya Google
Kama unatatizika kuunda nakala kwenye Hifadhi ya Google, thibitisha yafuatayo:
 • Una akaunti ya Google kwenye kifaa chako.
 • Umesakinisha huduma za Google Play kwenye kifaa chako.
 • Ikiwa unajaribu kuhifadhi nakala kupitia data ya mtandao wa simu, hakikisha una data kwa ajili ya huduma za WhatsApp na Google Play. Ikiwa huna hakika wasiliana na mtoa huduma wako.
 • Jaribu kuhifadhi nakala kwenye mtandao tofauti. Jaribu kuunganisha kwenye Wi-Fi ikiwa imeshindwa kuhifadhi nakala kupitia data ya mtandao wa simu.
Imeshindwa kurejesha nakala kutoka kwenye Hifadhi ya Google
Ikiwa unatatizika kurejesha nakala kutoka kwenye Hifadhi ya Google, thibitisha yafuatayo:
 • Unatumia nambari ya simu na akaunti ile ile ya Google ambapo ulikuwa umeweka nakala.
 • Kama unarejesha nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho, unatumia nenosiri au ufunguo sahihi.
 • Kuna nafasi ya kutosha kwenye kifaa chako ili kurejesha nakala hiyo.
 • Umesakinisha huduma za Google Play kwenye kifaa chako.
 • Betri ya kifaa chako imechajiwa kikamilifu au umeunganisha kifaa chako kwenye chanzo cha umeme.
 • Kifaa chako kina muunganisho mzuri na thabiti wa intaneti. Ikiwa inashindwa kurejesha kupitia data ya mtandao wa simu, tafadhali jaribu Wi-Fi.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La