Jinsi ya kubadilisha nambari yako ya simu


Kipengele cha kubadilisha nambari yako ya simu kinakuruhusu kubadilisha nambari ya simu inayohusishwa na akaunti yako ya WhatsApp kwenye simu hiyohiyo au mpya. Kabla hujabadilisha nambari yako ya simu:
 • Hakikisha kuwa nambari yako mpya ya simu inaweza kupokea SMS au simu na ina muunganisho wa selula amilifu.
 • Hakikisha nambari yako ya zamani ya simu sasa imesajiliwa kwenye WhatsApp. Unaweza kutafuta nambari yako ya simu iliyosajiliwa kwa kufungua WhatsApp, kisha kugusa Hiari zaidi > Mipangilio > gusa picha ya jalada lako.
Badilisha nambari ya simu kwenye simu hiyohiyo
Kama unabadilisha nambari yako ya simu na unatumia simu hiyohiyo, kwanza ingiza SIM kadi mpya yenye nambari mpya ya simu kwenye simu yako.
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Gusa Hiari zaidi
  > Mipangilio > Akaunti > Badilisha nambari > IFUATAYO.
 3. Ingiza nambari yako ya zamani kwenye uga wa kwanza na nambari mpya ya simu kwenye uga wa pili, zote kwenye mfumo kamili wa kimataifa.
 4. Gusa IFUATAYO.
  • Ukiwasha Waarifu waasiliani, unaweza kuchagua kama unataka kuwaarifu Waasiliani wote, Waasiliani ambao nina soga nao au Maalum.... Ukichagua Maalum..., utahitaji kutafuta au kuchagua waasiliani unaotaka kuwaarifu, kisha gusa alama hakikishi
   .
  • Vikundi vyako vya soga vitaarifiwa unapobadilisha nambari yako ya simu bila kijali kama ulichagua kuwaarifu waasiliani wako.
 5. Gusa IMEKAMILIKA.
 6. Utaulizwa kusajili nambari yako mpya ya simu. Jifunze zaidi kwenye makala haya.
Badilisha nambari ya simu kwenye simu mpya
Kama unahitaji kuhamisha historia yako ya soga, utahitaji kuunda chelezo la Google Drive kwenye simu yako ya zamani. Jifunze jinsi kwenye makala haya. Kama huundi chelezo kwa kutumia Google Drive, utahitaji kuhamisha chelezo lako kwa mkono, unaweza kujifunza jinsi ya kufanya hivyo kwenye makala haya.
Baada ya kubadilisha nambari yako ya simu kwenye simu yako ya zamani:
 1. Sakinisha WhatsApp kwenye simu yako mpya.
 2. Sajili nambari yako mpya ya simu.
 3. Rejesha chelezo yako.
Rasilimali zinazohusika:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La