Jinsi ya kutuma maudhui

Kutuma picha, video, nyaraka au anwani
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Bofya Ambatisha
  au
  , kisha bofya:
  • Picha na Video ili uchague picha au video kutoka kwenye kompyuta yako. Unaweza kutuma hadi picha au video 30 kwa mara moja na kuongeza muktasari kwa kila picha au video. Au, unaweza kuburura na kudondosha picha au video moja kwa moja katika sehemu ya maandishi. Kila video unayotuma haifai kuzidi MB 16.
  • Kamera ili upige picha kwa kamera ya kompyuta yako.
  • Hati ili uchague nyaraka kutoka kwenye kompyuta yako. Au, unaweza kuburura na kudondosha hati moja kwa moja katika sehemu ya maandishi. Ukubwa wa nyaraka unaoruhusiwa ni GB 2.
  • Anwani ili utume maelezo ya mawasiliano yaliyohifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako kupitia WhatsApp.
 3. Bofya Tuma
  au
  .
Kutuma ujumbe wa sauti
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Bofya maikrofoni
  au
  kisha uanze kuzungumza kwenye maikrofoni ya kompyuta yako.
 3. Ukimaliza, bofya Thibitisha
  ili utume ujumbe wa sauti.
Kumbuka: Wakati unarekodi ujumbe wa sauti, unaweza kubofya Ghairi
ili uache kurekodi.
Kuhifadhi picha au video kwenye kompyuta
 1. Boyfa picha au video unayotaka kuhifadhi.
 2. Bofya Pakua
  au
  . Ukiulizwa, bofya Hifadhi.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kutuma maudhui: Android | iPhone | KaiOS
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La