Jinsi ya kushiriki masasisho yako ya hali ya WhatsApp kwenye programu zingine

Kwenye Android na iPhone, una chaguo la kushiriki masasisho yako ya hali ya WhatsApp kwenye Hadithi za Facebook na programu zingine. Pata maelezo zaidi kuhusu faragha ya hali kwenye makala haya.
Kushiriki sasisho lako la hali kwenye Hadithi za Facebook
Ili kuwasha kipengele cha kushiriki hali yako ya WhatsApp kwenye Hadithi za Facebook, utahitaji kuthibitisha akaunti yako ya Facebook kwenye WhatsApp.
  1. Fungua WhatsApp.
  2. Gusa Hali.
    • Android: Gusa Chaguo zaidi > Faragha ya hali.
    • iPhone: GusaFaragha.
  3. Gusa Facebook > Anza > Kubali.
Baada ya kuthibitisha akaunti yako ya Facebook, unaweza kuunda sasisho la hali na kuchagua kuishiriki kwenye hadithi yako ya Facebook.
  1. Gusa Hali.
  2. Kuunda sasisho la hali kwenye: Android | iPhone
  3. Baada ya kuandika hali au maelezo mafupi kwenye picha, gusa Hali (Anwani).
  4. Chagua hadhira gani ungependa ione sasisho lako la hali. Ili kushiriki sasisho lako la hali kwenye hadithi yako ya Facebook, gusa Shiriki kwenye hadithi ya Facebook kila wakati.
Kuzima kipengele cha kushiriki hali kwenye Facebook
  1. Fungua WhatsApp.
  2. Gusa Hali.
    • Android: Gusa Chaguo zaidi > Faragha ya hali.
    • iPhone: GusaFaragha.
  3. Gusa Facebook.
  4. Gusa Zima kipengele cha kushiriki hali kwenye Facebook > Zima.
Kushiriki sasisho lako la hali kwenye programu zingine
  1. Fungua WhatsApp.
  2. Gusa Hali.
  3. Kuunda sasisho la hali kwenye: Android | iPhone
  4. Una chaguo mbili za kushiriki kulingana na ikiwa unataka kushiriki sasisho jipya la hali au la zamani:
    • Kushiriki sasisho jipya la hali: Chini ya Hali yangu, gusa Shiriki (
      au
      ). Tafadhali kumbuka kuwa chaguo la Kushiriki hutoweka mara tu unapoenda kwenye kichupo kingine.
    • Kushiriki sasisho la zamani la hali: Gusa Hali Yangu kwenye iPhone au Zaidi
      na Hali yangu kwenye Android. Kisha, gusa Zaidi (
      au
      ) karibu na sasisho la hali unalotaka kushiriki, kisha uguse Shiriki.
  5. Gusa programu unayotaka kushiriki sasisho lako la hali.
Rasilimali
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La